Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 55 TWAPANDA MAPEMA nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 55 TWAPANDA MAPEMA nyimbo za wokovu

 

1
Twapanda mapema
Na mchana kutwa
Mbegu za fadhili
Hata jioni,
Twangojea sasa
Siku za kuvuna;
Tutashangilia
Wenye mavuno.

Wenye mavuno,
Wenye mavuno,
Tutashangilia
Wenye mavuno,
Wenye mavuno,
Wenye mavuno,
Tutashangilia
Wenye mavuno.

2
Twapanda mwangani
Na kwenye kivuli
Tusishindwe
Na baridi na pepo
Punde itakwisha
Kazi yetu hapa
Tutashangilia
Wenye mavuno.

3
Twapanda kwa Bwana
Mbegu kila siku.
Tujapoona taabu
Na huzuni;
Tuishapo shinda
Atatupokea;
Tutashangilia
Wenye mavuno.

Exit mobile version