Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 53 NAPENDA KUHUBIRI nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 53 NAPENDA KUHUBIRI nyimbo za wokovu

 

1
Napenda kuhubiri
Habari ya Yesu,
Ya Bwana wa fahari
Na pendo zake kuu.
Kuhubiri napenda
Kwa hali na mali:
Mwenyewe nimeonja,
Najua ni kweli.

Napenda kuhubiri
Kisa cha Bwana Yesu,
Ya Bwana wa fahari
Na pendo zake kuu.

2
Napenda kuhubiri
Mambo ya ajabu
Na tukiyafikiri
Yapita dhahabu.
Kuhubiri napenda
Ya yaliyonifaa:
Nami sana napenda
Hayo Kukwambia.

3
Napenda kuhubiri,
Hunifurahisha
Tamu yake habari
Haiwezi kwisha.
Napenda kuhubiri
Wagizani nao;
Hawana muhubiri
Wa kweleza chuo

4
Kuhubiri napenda
Hata wajuao;
Kusikia hupenda
Kama wenzi wao.
Nako kwenye fahari
Nikiimba wimbo.
Nitaimba habari
Ya Mwokozi huyo

Exit mobile version