Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 52 NIPE BIBLIA nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 52 NIPE BIBLIA nyimbo za wokovu

 

1
Nipe Biblia nyota ya furaha,
wapate nuru wasafirio;
Hakuna la Kuzuia amani,
Kwani Yesu alituokoa.

Nipe Biblia neno takatifu,
Nuru yake itaniongoza;
Sheria na ahadi na upendo,
hata mwisho vitaendelea.

2
Nipe Biblia nihuzunikapo
ikinijaza moyoni dhambi;
Nipe neno zuri la Bwana Yesu,
Nimwone Yesu Mwokozi wangu.

3
Nipe Biblia nipate kuona,
Hatari zilizo duniani;
Nuru ya neno lake Bwana Yesu,
Itaangaza njia ya kweli.

4
Nipe Biblia taa ya maisha;
Mfariji tunapofiliwa;
Unionyeshe taa ya mbinguni,
Nione utukufu wa Bwana.

Exit mobile version