Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 51 KUWA NA YESU MWOKOZI nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 51 KUWA NA YESU MWOKOZI nyimbo za wokovu

 

1
Yesu Mwokozi, kwa hakika,
Hunipa furaha na amani;
Mrithi wa wokovu wake,
Natakaswa kwa damu yake.

Habari hiyo wimbo wangu,
Daima nitamsifu Yesu.
Habari hiyo wimbo wangu,
Daima nitamsifu Yesu.

2
Nilijitoapo nina raha,
Na kwa imani namwona Bwana;
Aniletea malaika,
Wananilinda, niokoke.

3
Hali na mali anaitwaa,
Katika Yesu Nabarikiwa;
Nikimngoja kwa subira,
Wema wake unanitosha.

Exit mobile version