Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 5 NA TUMWABUDU nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 5 NA TUMWABUDU nyimbo za wokovu

 

1
Na tumwabudu huyo mfalme,
Sifa na nguvu zake zivume,
Ni ngao ni ngome yeye milele,
Ndizo sifa zake kale na kale.

2
Tazameni ulimwengu huu,
Ulivyoumbwa ajabu kuu,
Sasa umewekwa pahali pake,
Hata utimize majira yake.

3
Kwa ulinzi wako kwetu Bwana,
Twakushukuru umwema sana,
Hupewa chakula kila kiumbe,
Kila kitu kina mahali pake.

4
Wanadamu tu wanyonge sana,
Twakutumaini wewe Bwana,
Kamwe haupungui wako wema,
Mkombozi wetu rafiki mwema.

Exit mobile version