Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 4 JINA LA YESU SALAMU nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 4 JINA LA YESU SALAMU nyimbo za wokovu

 

1
Jina la Yesu salamu,
Lisujudieni,
Ninyi mbinguni hukumu,
Na enzi mpeni,
Ninyi mbinguni hukumu
Na enzi, mpeni.

2
Enzi na apewe kwenu,
Watetea dini,
Mkuzeni Bwana wenu,
Na enzi mpeni
Mkuzeni Bwana wenu
Na enzi, mpeni

3
Enyi mbegu ya rehema,
Nanyi msifuni,
Mmeponywa kwa neema,
Na enzi mpeni.
Mmeponywa kwa neema,
Na enzi mpeni.

4
Wenye dhambi kumbukeni
Ya msalabani.
Kwa furaha msifuni,
Na enzi mpeni.
Kwa furaha msifuni,
Na enzi mpeni.

5
Kila mtu duniani,
Msujudieni,
Kote kote msifuni,
Na enzi mpeni
Kote kote msifuni
Na enzi, mpeni

6
Sisi na wao pamoja,
Tumumo sifani,
Milele sifa ni moja,
Ni enzi mpeni,
Milele sifa ni moja
Ni enzi, mpeni.

Exit mobile version