Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 36 SIKU KUU nyimbo za wokovu
1
Ni siku kuu siku ile
ya kumkiri Mwokozi!
Moyo umejaa tele,
kunyamaza hauwezi.
Siku kuu! Siku kuu!
ya kuoshwa dhambi zangu kuu!
Hukesha na kuomba tu,
Ananiongoza miguu.
Siku kuu! Siku kuu!
Ya kuoshwa dhambi zangu kuu
2
Tumekwisha kupatana,
mimi wake, yeye wangu,
Na sasa nitamwandama,
nikiri neno la Mungu.
3
Moyo tulia kwa Bwana,
kiini cha raha yako;
Huna njia mbili tena;
uwe naye, yote ndako.