Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 35 NIMEKOMBOLEWA NA YESU nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 35 NIMEKOMBOLEWA NA YESU nyimbo za wokovu

 

1
Nimekombolewa na Yesu
Na sasa nimefurahi;
Kwa bei ya mauti yake
Mimi ni mtoto wake.

Kombolewa!
Nakombolewa na damu;
Kombolewa!
Mimi mwana wake kweli.

2
Kukombolewa nafurahi,
Kupita lugha kutamka;
Kulionyesha pendo lake,
Mimi ni mtoto wake.

3
Nitamwona Mfalme wangu
Katika uzuri wake;
Ambaye najifurahisha
Katika torati yake.

4
Najua taji imewekwa
mbinguni tayari kwangu;
Muda kitambo atakuja,
ili alipo, niwepo.

Exit mobile version