Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 29 YESU UNIPENDAYE nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 29 YESU UNIPENDAYE nyimbo za wokovu

 

1
Yesu, Unipendaye
kwako nakimbilia,
Ni wewe utoshaye
mwovu akinijia.
Yafiche ubavuni
mwako maisha yangu;
Nifishe bandarini,
wokoe moyo wangu.

2
Ngome nyingine sina;
nategemea kwako,
Usinitupe Bwana,
nipe neema yako;
Ninakuamania,
mwenye kuniwezesha;
Shari wanikingia,
vitani wanitosha.

3
Nakutaka Mpaji,
vyote Napata kwako;
Niwapo muhitaji,
utanijazi vyako;
Nao waangukao
wanyonge wape nguvu;
Poza wauguao,
uongoze vipofu.

4
Bwana umeniosha
moyo kwa damu yako;
Neema ya kutosha
yapatikana kwako;
Kwako Bwana naona
kisima cha uzima;
Mwangu moyoni, Bwana,
Bubujika daima.

Exit mobile version