Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 28 JINA LA THAMANI nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 28 JINA LA THAMANI nyimbo za wokovu

 

1
Jina Lake Yesu tamu,
Lihifadhi moyoni;
Litakufariji ndugu,
Enda nalo po pote.

Jina la Thamani,
(Thamani) (Thamani)
Tumai la dunia
Jina la Thamani
Furaha ya mbinguni.

2
Jina la Yesu lafaa
kama ngao vitani.
Majaribu yakisonga,
Omba kwa jina hili.

3
Jina hili la thamani
Linatufurahisha,
Anapotukaribisha,
Na tunapomwimbia.

4
Mwisho wa safari yetu
Tutakapo msujudu,
Jina hili tutasifu
Furaha ya mbinguni.

Exit mobile version