Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 27 TENA, MWOKOZI, TWALITUKUZA JINA LAKO nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 27 TENA, MWOKOZI, TWALITUKUZA JINA LAKO nyimbo za wokovu

 

1
Tena, Mwokozi, twalitukuza
Jina lako lenye kupendeza,
Twangojea neno la amani,
Kabla hatujakwenda nyumbani.

2
Tupe amani njiani mwetu,
Wewe u mwanzo, umwisho wetu;
Dhambini kamwe isiingie
Midomo ikutajayo wewe.

3
Utupe amani usiku huu,
Ili gizani kuwe nuru kuu.
Tulinde kwa kuwa kwako Bwana,
Usiku ni sawa na mchana.

4
Tupe amani ulimwenguni
Ndiyo dawa yetu majonzini;
Na ikitwita sauti yako,
Tupe amani milele kwako.

Exit mobile version