Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 26 TUTOKAPO TUBARIKI nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 26 TUTOKAPO TUBARIKI nyimbo za wokovu

 

1
Tutokapo tubariki,
Utupe kufurahi;
Tuwe na upendo wako,
Neema ya kushinda.
Nawe utuburudishe
Tukisafiri chini.

2
Twatoa sifa, shukrani
Kwa neno la Injili;
Matunda yake wokovu
Yaonekane kwetu;
Daima tuwe amini
Kwa kweli yako, Bwana.

3
Siku zetu zikizidi
Tuzitoe kwa Yesu;
Tuwe na nguvu moyoni
Tusichoke njiani;
Hata tutakapoona
Utukufu wa Bwana.

Exit mobile version