Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 25 TAJI MVIKENI nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 25 TAJI MVIKENI nyimbo za wokovu

 

1
Taji mvikeni
Taji nyingi sana,
Kondoo mwake kitini,
Bwana wa mabwana;
Nami tamsifu
Alikufa kwangu,
Ni mfalme mtukufu,
Seyidi wa mbingu

2
Taji mvikeni
Mwana wa Bikira;
Anazovaa kichwani,
Aliteka nyara;
Shilo wa manabii
Mchunga wa watu
Shina na tanzu ya Yese
Wa Bethilehemu.

3
Taji mvikeni
Bwana wa Mapenzi;
Jeraha zake ni shani
Ni vito vya enzi,
Mbingu haina Hata malaika
Awezae kuziona
pasipo kushangaa!

4
Taji mvikeni
Bwana wa salama;
Kote-kote duniani
Vita vitakoma;
Nayo enzi yake
Itaendelea,
Chini ya miguu yake,
Maua humea.

Exit mobile version