Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 24 JINA LAKE YESU TAMU nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 24 JINA LAKE YESU TAMU nyimbo za wokovu

 

1
Jina lake Yesu tamu,
Tukilisikia,
Hutupoza, tena hamu
Hutuondolea.

2
Roho iliyoumia
Kwalo hutibika,
Chakula, njaa pia:
Raha, tukichoka.

3
Jina hili ni msingi,
Ngao, ngome, mwamba,
Kwa hili Napata ungi,
Kwangu ni akiba.

4
Yesu, Mchunga, Rafiki,
Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, Mwisho, na Amina,
Mali yangu yote!

5
Moyo wangu hauwezi
Kukusifu kweli;
Ila sifa zangu hizi,
Bwana, zikubali.

Exit mobile version