Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 22 USINIPITE MWOKOZI nyimbo za wokovu
1
Usinipite, Mwokozi,
Unisikie;
Unapozuru wengine,
Usinipite.
Bwana, Bwana,
Unisikie;
Unapozuru wengine,
Usinipite.
2
Kiti chako cha rehema,
Nakitazama;
Magoti napiga pale,
Nisamehewe.
3
Sina ya kutegemea,
Ila wewe tu;
Uso wako uwe kwangu:
Nakuabudu.
4
Wewe tu u mfariji:
Sina mbinguni,
Wala duniani pote,
Bwana mwingine.