Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 207 MWOKOZI WANGU ANIPENDA nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 207 MWOKOZI WANGU ANIPENDA nyimbo za wokovu

 

1
Mwokozi wangu alinipenda,
Maovu hayanitengi naye,
Alijitoa, kuniponya,
Sasa mimi wake.

Mimi wake kabisa,
Naye Yesu wangu,
Si kwa wakati huu tu,
Bali na milele.

2
Dhambini nilijidhili sana,
Yesu akaja kunikomboa,
Akanitoa sumbukoni,
Sasa mimi wake.

3
Furaha nyingi moyoni mwangu,
Bwana Yesu kunifanya huru,
Kunitwaa kwa damu yake,
Sasa mimi wake.

Exit mobile version