Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 195 MSINGI WA KANISA nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 195 MSINGI WA KANISA nyimbo za wokovu

 

1
Msingi wa Kanisa
Ndiye Yesu Bwana;
Kiumbe chake kipya
Akipenda sana;
Kutaka ‘kitafuta
Alishuka chini,
Naye kwa haja yake,
Akafa Mtini.

2
Lina kila kabila
Kisha ndiyo moja
Wokovu wake una
Mwokozi mmoja;
Uzazi ni umoja,
Moja tumaini.
Chakula ni kimoja,
Moja tumaini.

3
Watu hustaajabu
Kwa mashaka yote
Yaipatayo nje
Hata ndani mwote;
Ila watakatifu
Humwomba, wakikesha
Usiku ni kilio,
Asubuhi raha.

4
Mashaka na taabu
Hata vita vyake,
Vyangoja matimizo
Ya amani yake,
Ndipo kwa macho yetu
Twone utukufu
Kanisa ya kushinda
Itastarehe juu.

Exit mobile version