Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 188 WIMBI LITAKASALO nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 188 WIMBI LITAKASALO nyimbo za wokovu

 

1
Wimbi la damu ya Yesu
Linatutakasa;
Aliumia kusudi
Tupate uzima.

Wimbi la damu naona,
Naingia, natakaswa!
Bwana asifiwe sana,
Hutakasa, hutakasa.

2
Damu inasema kwangu,
Nasikia mvuto;
Inasema, moyo wangu
Hutakaswa nayo.

3
Naondoka kutembea
Kwa nuru ya mbingu;
Mavazi yamesafishwa;
Moyoni ni Yesu.

4
Neema ni ya ajabu,
Kutakaswa ndani!
Na kuwa naye Yesu tu,
Aliye Mwokozi.

Exit mobile version