Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 180 PANA MAHALI PAZURI MNO nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 180 PANA MAHALI PAZURI MNO nyimbo za wokovu

 

1
Pana mahali pazuri mno,
Twapaona kwa mbali sasa;
Baba Yetu angoja pale,
Amepanga makao yetu.

Kitambo tu bado,
Tutakutana ng’ambo pale.
Kitambo tu bado,
Tutakutana ng’ambo pale.

2
Tutaimba pale kwa moyo,
Nyimbo tamu za wenye heri
Na rohoni hatutaona
Tena haja ya kupumzika.

3
Kwa Baba yetu mkarimu
Tutatoa shukrani sana,
Kwa kipaji cha pendo lake
Na Baraka anazotupa.

Exit mobile version