Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 178 UKIONGONI MWA YORDANI nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 178 UKIONGONI MWA YORDANI nyimbo za wokovu

 

1
Ukingoni mwa Yordani
Ninaangalia
Bara nzuri ya Kanaani,
Ninayotamani.

Tutakaa pamoja na Yesu,
Katika pwani yenye raha;
Tutaimba wimbo wa Musa na
Kondoo, Milele hata milele.

2
Bara ile ina nuru,
Nuru ya milele;
Kristo, Jua, hutawala,
Hufukuza giza.

3
Nitapafikia lini
Na kubarikiwa,
Penye ufalme wa Baba,
Na kumwona uso?

4
Furaha yangu rohoni
Ni kuchukuliwa;
Siyaogopi mawimbi
Katika Yordani.

Exit mobile version