Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 175 USO KWA USO nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 175 USO KWA USO nyimbo za wokovu

 

1
Nitaonana na Yesu,
Uso kwa uso kweli;
Siku ile shangwe tele
Nikimwona Mwokozi.

Tutaonana kwa macho,
huko kwetu mbinguni;
Na kwa utukufu wake,
nitamwona milele.

2
Sasa siwezi kujua
Jinsi alivyo hasa,
Bali atakapokuja,
Nitamwona halisi.

3
Mbele yake yafukuzwa
Machozi na huzuni;
Kipotovu kitanyoshwa,
Fumbo litafumbuka.

4
Uso kwa uso! Hakika
Palepale furaha;
Nitafurahi kabisa
Nikimwona Mwokozi.

Exit mobile version