Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 174 TUKIMNGOJEA nyimbo za wokovu
1
Sijui atakapokuja,
Mchana au usiku;
Labda sa-a ya alasiri,
Pengine ni alfajiri
Hutwambia tuwe tayari,
Ta-a zetu tusizime;
Ili ajapo atukute;
Tuwe tukimngoja Yeye.
Tu-kimngoje–a,
(Kukesha, tunakungoja Wewe)
Tu—kimngoje–a,
(Kukesha tunakungoja Wewe)
Tu—kimngoje–a,
(Kukesha tunakungoja Wewe)
Twakesha, twamngoja Yeye.
2
Nakumbuka huruma zake,
Bei ya wokovu wetu:
Aliacha nyumba tukufu
Awafilie wabaya.
Ninadhani itampendeza,
Kama sisi watu wake,
Tukionyesha pendo letu,
Tuwe tukimngoja Yeye.
3
Ee Yesu, Mwokozi mpendwa,
Wajua nalihifadhi
Tumaini la kukuona,
La kukaribishwa nawe.
Ukija kwa watu wengine,
Kama mhukumu wao,
Kwangu utakuwa rafiki,-
Nakesha nakungojea.