Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 170 JINA LANGU LIMEANDIKWA JE? nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 170 JINA LANGU LIMEANDIKWA JE? nyimbo za wokovu

 

1
Sitafuti mali,
Wala utajiri;
Nataka kwa yakini
Nipate Mwokozi.
Chuoni mwa Ufalme,
Niambie Yesu.
Jina langu yakini
Limeandikwa, je?

Limeandikwa, je?
Jina langu huko?
Kitabuni mbinguni,
Limeandikwa je?

2
Dhambi zangu ni nyingi,
Ni kama mchanga.
Lakini damu yako,
Mwokozi, yatosha;
Kwani umeahidi;
Zijapo nyekundu
Zitakuwa nyeupe
Ilivyo theluji.

3
Mji mzuri sana,
Wa majumba makuu,
Walipo malaika,
Mji bila ovu;
Wakaapo walio
Na mavazi safi,
Limeandikwa sasa,
Jina langu huko?

Exit mobile version