Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 169 TUTASHINDAJE HUKUMUNI? nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 169 TUTASHINDAJE HUKUMUNI? nyimbo za wokovu

 

1
Hapo Yesu atakapoita
mataifa mbele yake,
Tutashindaje kwenye hukumu
mbele ya kiti cha enzi?

Atakusanya ngano ghalani,
atatupa mbali makapi;
Tutashindaje hukumuni
siku ya kiyama?

2
Je, tutasikia neno tamu;
‘Vema, wewe mtumwa mwema’
Ama wenye uchungu na hofu
tutakatazwa ufalme?

3
Atakubali tu kwa furaha
watoto wake wapendwa,
Atawapa mavazi meupe,
wakae kitini peke.

4
Hivyo tukeshe, nasi tungoje,
wenye taa zinazowaka;
Tutakapoitwa arusini
tuwe tayari kumlaki.

5
Roho ikielekea mbinguni
twangoja wenye saburi,
Hata safari yetu iishe,
tukae kwake milele.

Exit mobile version