Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 167 YU HAI, YU HAI nyimbo za wokovu
1
Yesu Bwana Mwokozi
Aishi milele,
Najua kwamba Yupo
Pamoja na mimi;
Sauti nasikia,
Rehema naona;
Wakati namhitaji,
Yupo nami.
Yu hai, Yu hai,
Yu hai Bwana Yesu!
Atembea, Azungumza
Nami siku zote.
Yu hai, Yu hai,
Kutoa uzima!
Hivi ndivyo nijuavyo,
Yu hai ndani yangu!
2
Ulinzi Wake upo
Naona dhahiri,
Miguu ichokapo,
Sikati tama.
Najua an’ongoza
Kupita dhoruba,
Siku ya kuja kwake
Nitamwona.