Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 165 AHADI TAMU nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 165 AHADI TAMU nyimbo za wokovu

 

1
Ahadi tamu kwa waamini,
Tazama nakuja upesi sana.
Uwe imara, hatari kubwa;
Ndugu usilale, bali ukeshe.

Uihifadhi imani yako,
Dunia mpya itatolewa,
Njoo ingia furaha yangu;
Taji zinangoja; Uwe imara.

2
Tutakesha na kutoa sala;
Atakuja kama mwivi kwa wengi;
Ya kwamba yu karibu twajua,
Ila hatujui ni siku gani.

3
Tunategemea Neno lake,
Ambalo latangaza kuja kwake,
Tumaini letu ni ahadi;
Naja karibuni, uwe imara.

Exit mobile version