Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 164 MISHALE YA NURU nyimbo za wokovu
1
Unakaribia wakati
Wa Kuja kwa Yesu
Atawachukua watu
Wake Nyumbani juu.
Tunaiona mishale ya nuru
Inayopenya giza;
Tunaiona mishale ya nuru
Ya ufufuo
2
Injili inatangazwa
Pote Kwa mataifa;
Bwana wa Arusi
Atakuja Na tarumbeta.
3
Pamoja na malaika
Zake Bwana arudi,
Awapeleke waaminifu
Wasife tena.
4
Wapenzi waliotengwa
Kale Watakutana;
Machozi yao wenye
Huzuni Yatafutika.