Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 160 WATAKATIFU KESHENI nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 160 WATAKATIFU KESHENI nyimbo za wokovu

 

1
Watakatifu kesheni,
Nguvu za mbingu zagonga;
Washeni taa tayari
Kwa kurudi kwake Bwana.

Yuaja, Yesu Mfalme,
Yuaja mwenye fahari,
Yesu yuaja enzini.
Karibu Yesu uje.

2
Piga mbiu, tangazeni
Habari ya ukombozi
Ya Mponya wa upendo
Nayo nguvu ya samaha.

3
Falme nyingi zaangushwa,
Panda ya saba hulia;
Tangaza neema yake
Kabla ya kupita saa.

4
Mataifa yapotea,
Nchi zajaa uchungu:
Kristo anaharakisha.
Unabii unatimizwa.

5
Wenye dhambi njoni sasa,
Kristo awapatanishe,
Mbio twaeni neema,
Kitambo muda waisha.

Exit mobile version