Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 155 NJIANI HUNIONGOZA nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 155 NJIANI HUNIONGOZA nyimbo za wokovu

 

1
Njiani huniongoza
Yesu wangu, Mwokozi:
Rehema hatapunguza,
Milele Kiongozi.
Ina raha kwandamana
Duniani daima:
Nijaposumbuka sana,
Yeye hutenda vyema.

2
Njiani huniongoza
Hupunguza matata;
Nikiugua hupoza,
Na njaani nashiba.
Lichokapo guu langu
Nguvu zikapungua,
Jiwe lilo mbele yangu
Hunibubujika.

3
Njiani huniongoza
Kwa pendo zilizo kuu,
Mwisho atanituliza
Kwake Baba yangu juu.
Nikivikwa kutokufa,
Nikae na Mwokozi,
Nitamsifu sana; sifa:
Kweli ni Kiongozi

Exit mobile version