Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 152 KARIBU NA WEWE, MUNGU WANGU nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 152 KARIBU NA WEWE, MUNGU WANGU nyimbo za wokovu

 

1
Karibu na wewe,
Mungu wangu;
Karibu zaidi
Bwana Wangu.
Siku zote niwe
Karibu na wewe.
Karibu zaidi,
Mungu wangu.

2
Mimi nasafiri
Duniani,
Pa kupumzika
Sipaoni,
Nilalapo niwe
Karibu na wewe;
Karibu zaidi,
Mungu wangu.

3
Yote unipayo
Yanivuta;
Pa kukaribia
Nitapata;
Na nielekezwe,
Karibu na wewe;
Karibu zaidi,
Mungu wangu.

4
Na kwa nguvu zangu
Nikusifu;
Mwamba, uwe maji
Ya wokovu.
Mashakani niwe,
Karibu na wewe;
Karibu zaidi,
Mungu wangu.

5
Na nyumbani mwa juu,
Baba yangu
Nikinyakuliwa
Toka huko.
Kwa furaha niwe
Pamoja na wewe.
Karibu zaidi,
Mungu wangu.

Exit mobile version