Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 151 HUNIONGOZA MWOKOZI nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 151 HUNIONGOZA MWOKOZI nyimbo za wokovu

 

1
Huniongoza Mwokozi,
Ndipo nami hufurahi,
Niendapo pote napo,
Ataniongoza papo.

Kuongoza hunishika;
Kwa mkono wa hakika;
Nitaandamana naye
Kristo aniongozaye.

2
Pengine ni mashakani
Nami pengine rahani;
Ni radhi, ijayo yote,
Yupo nami siku zote.

3
Mkono akinishika
Kamwe sitanungunika;
Atakachoniletea
Ni tayari kupokea.

4
Nikiisha kazi chini
Sitakimbia mauti;
Kushinda ni ya hakika
Nikiongozwa na Baba.

Exit mobile version