Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 15 NENA MUNGU nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 15 NENA MUNGU nyimbo za wokovu

 

1
Nena rohoni Yesu,
Nena kwa upole
Sema kwangu kwa pendo,
Huachwi upweke.
Fungua moyo wangu,
Nisikie mara;
Jaza roho na sifa,
Sifa zako Bwana.

Kila siku unene,
Vile kwa upole.
Nong’oneza kwa pole
Wa upendo:
Daima utashinda,
Uhuru ni wako.
Nisikie maneno:
Huachwi upweke.

2
Nena kwa wana wako,
Waonyeshe njia,
Wajaze kwa furaha,
Fundisha kuomba;
Wajifunze kutoa
Maisha kamili,
Wahimize ufalme,
Tumwone mwokozi.

3
Nena kama zamani,
Ulipoitoa
Sheria takatifu:
Niiweke pia;
Nipate kutukuza
Wewe Mungu wangu,
Mapenzi yako tena,
Daima kusifu.

Exit mobile version