Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 147 UISHI NDANI YANGU nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 147 UISHI NDANI YANGU nyimbo za wokovu

 

1
Tawala ndani yangu,
Ee Yesu, Mfalme.
Uwe kwangu majibu
Kwa maswali yangu;
Uishi ndani yangu,
Wenye, mwongozi
Utumishi ni wangu,
Wako utukufu.

2
Hekalu nimetoa,
Umelisafisha;
Sasa fahari yako
Imulike ndani;
Dunia iwe kimya,
Mwili sasa uwe
Mtumwa mtulivu
Wa kukutii tu.

3
Viungo vyake mwili,
Vyote vikungoja
Tayari vikiitwa
Kwenda, kusimama;
Bila manung’uniko
Au malaumu,
Au kusumbuliwa,
Pasipo majuto.

4
Niwe na utulivu
Pasipo haraka;
Tayari kungojea
Maagizo yako.
Tawala ndani yangu.
Ee Yesu, Mfalme,
Uwe kwangu majibu
Kwa maswali yote.

Exit mobile version