Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 144 NI WAKO BWANA nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 144 NI WAKO BWANA nyimbo za wokovu

 

1
Ni wako Bwana, Ninasikia,
Unaponena nami,
Lakini kweli nataka kwako
nizidi kusongea.

Bwana vuta, (vuta) Nije nisonge,
Sana kwako mtini,
Bwana vuta, vuta, Nije nisonge,
Kwa damu ya thamani.

2
Niweke sasa, Nikatumike,
Kwa nguvu za neema,
Uyapendayo nami nipende
nizidi kukwandama.

3
Nina furaha, Tele kila saa,
Nizungumzapo nawe,
Ninanena kama kwa rafiki
nikipiga magoti.

Exit mobile version