Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 139 ULINIIMBIE TENA nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 139 ULINIIMBIE TENA nyimbo za wokovu

 

1
Uliniimbie tena,
Neno la uzima;
Uzuri wake nione,
Neno la Uzima;
Neno hili zuri,
Lafundisha Kweli;

Maneno ya uzima
Ni maneno mazuri,
Maneno ya uzima
Ni maneno mazuri.

2
Kristo anatupa sote,
Neno la uzima;
Mwenye dhambi asikie
Neno la uzima;
Latolewa bure,
Tupate wokovu;

3
Neno tamu la injili,
Neno la uzima;
Lina amani kwa wote
Neno la uzima;
Litatutakasa,
Kwa haki ya Mwana;

Exit mobile version