Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 138 NITAKUANDAMA KOTE nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 138 NITAKUANDAMA KOTE nyimbo za wokovu

 

1
Nitakuandama Kote,
Nitakapoagizwa,
Wewe ukiniongoza
Nami nitaandama.

Nitakuandama kote,
Naam, ulinifia;
Kwa neema yako Bwana
Napenda kuandama.

2
Njia ijapoparuza
Kwa miiba na fujo,
Ulitangulia mbele
Nami nitaandama.

3
Nijapokuta taabu
Na majaribu kote,
Nakumbuka shida yako,
Nami nitaandama.

4
Nijapoona ukiwa
Na mateso makali
Wewe uliyatikiza
Nami nitaandama.

5
Ijapo wanipeleka
Vilindini mwa giza,
Wewe uliyatikiza
Nami nitaandama.

Exit mobile version