Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 131 BABA ANILINDA nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 131 BABA ANILINDA nyimbo za wokovu

 

1
Namtegemea Mungu niwapo
Humo barani na baharini,
Yeye wa mbinguni anilinda
Baba wa mbinguni anilinda.

Namwamini, Mungu anitunza
Milimani au baharini
Moyo wangu aulinda,
Baba wa mbinguni anilinda

2
La Waridi alinawirisha,
Na huyo tai juu angani,
Nani kweli ananilinda,
Baba wa mbinguni anilinda.

3
Tunduni mwa simba namwamini,
Kwenye vita ama gerezani,
Motoni na furikoni,
Baba wa mbinguni anilinda.

4
Bondeni mwa giza na upweke,
Mchunga wangu yuanilinda,
Kwa upole aniongoza,
Baba wa mbinguni anilinda.

Exit mobile version