Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 128 TAAMINI NITII PIA nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 128 TAAMINI NITII PIA nyimbo za wokovu

 

1
Namwandama Bwana
Kwa alilonena,
Njia zangu huning’azia;
Na nikimridhisha
Atanidumisha,
Taamini nitii pia.

Kuamini,
Njia pweke ni hii
Ya furaha kwa Yesu:
Amini ukatii.

2
Giza sina kwangu,
Wala hata wingu,
Yeye mara huviondoa;
Oga, wasiwasi,
Sononeko, basi;
Huamini nitii pia.

3
Masumbuko yote,
Sikitiko lote;
Kwa mapenzi hunilipia;
Baa, dhara, dhiki,
Vivyo hubariki,
Taamini nitii pia.

4
Mimi sitajua
Raha sawasawa
Ila yote Yesu kumtoa;
Napata fadhili
Na radhi kamili,
Taamini nitii, pia.

5
Nitamfurahia
Na kumtumaini,
Majumbani na njia-njia;
Agizo natenda;
Nikitumwa hwenda,
Huamini, nitii pia.

Exit mobile version