Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 123 YESU KWA IMANI nyimbo za wokovu
1
Yesu kwa imani,
Nakutumaini,
Peke yako;
Nisikie sasa,
Na kunitakasa,
Ni wako kabisa
Tangu leo.
2
Nipe nguvu pia
Za kusaidia
Moyo wangu;
Ulikufa wewe,
Wokovu nipewe,
Nakupenda wewe
Bwana wangu.
3
Hapa nazunguka
Katika mashaka,
Na matata;
Palipo na giza
Utaniongoza,
Hivi nitaweza
Kufuata.