Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 117 WAMWENDEA YESU? nyimbo za wokovu
1
Wamwendea Yesu kwa kusafiwa.
Kuoshwa kwa damu ya Kondoo?
Je, neema yake yatumwagiwa?
Waoshwa kwa damu ya Kondoo?
Kuoshwa, kwa damu
itutakasayo ya Kondoo?
Ziwe safi nguo nyeupe sana;
Waoshwa kwa damu ya Kondoo?
2
Wamwandama daima Mkombozi.
Waoshwa kwa damu ya Kondoo?
Yako kwa Msulubiwa mavazi?
Waoshwa kwa damu ya Kondoo?
3
Atakapokuja Bwana-arusi
Uwe safi katika damu!
Yafae kwenda mbinguni mavazi:
Yaoshwa kwa damu ya Kondoo?
4
Yatupwe yalipo na takataka;
Uoshwe kwa damu ya Kondoo:
Huoni kijito chatiririka
Uoshwe kwa damu ya Kondoo?