Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 113 BUBUJIKO nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 113 BUBUJIKO nyimbo za wokovu

 

1
Damu imebubujika,
Ni ya Imanweli,
Wakioga wenye taka,
Husafiwa kweli.

2
Ilimpa kushukuru
Mwivi mautini;
Nami nisiye udhuru,
Yanisafi ndani.

3
Kondo-o wa kuuawa,
Damu ina nguvu,
Wako wote kuokoa
Kwa utimilivu.

4
Bwana, tangu damu yako
Kunisafi kale,
Nimeimba sifa zako,
‘Taimba milele.

5
Bwana, umenikirimu
Nisiyestahili
Kwa damu yako, sehemu
Ya mali ya kweli.

6
Nikubali kukwimbia
Mbinguni milele.
Mungu nitamsifia
Jina lako pweke.

Exit mobile version