Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 106 HUNA KITU KWA YESU? nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 106 HUNA KITU KWA YESU? nyimbo za wokovu

 

1
Ukitafuta mali,
Huna wasaa kwa Yesu?
Kwa matendo ya haki
Huna wasaa kwa Yesu?
Anasa za dunia,
Mambo yako ya raha
Haya unatafuta;
Huna wasaa kwa Yesu?

2
Mambo yanakusonga;
Kwake huna nafasi?
Watekwa na dunia,
Kwake huna nafasi?
Humwoni m-langoni,
Anapopiga hodi?
Daima hukusihi;
Kwake huna nafasi.

3
Sa-a ni za thamani,
kwake hamnayo kazi
Wala hamfanyi bidii,
Kwake hamnayo Kazi?
Hamkufikia kwao
Waliomo shimoni
Na waliopotea?
Kwake hamnayo kazi?

4
Na wazaa majani tu?
Huna tunda kwa Yesu?
Mikono i mitupu,
Huna tunda kwa Yesu?
Huna chembe kwa ghala
Kazi yako kuilipa;
Wala huna furaha
Unapomwona Yesu?

Exit mobile version