Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 105 MCHUNGAJI MPENZI nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 105 MCHUNGAJI MPENZI nyimbo za wokovu

 

1
Mchungaji mpenzi
Hukuita uje,
Katika zizi lake
Panapo salama:
Akina wanawake
Waume vijana,
Yesu aliye kweli
Huwaita kwake.

Huita kwa moyo
Wa huruma,
‘Uliyepotea
Uje kwangu.
Hivi kukungoja
Anadumu
Bwana Yesu
Mchunga.

2
Akatoa maisha
Kwa ajili yetu;
Ataka wapotevu
Waje kwake sasa;
Tusijihatarishe
Kwake tu salama;
Sikia wito wake
Mchungaji wetu.

3
Tusikawie tena,
Adui shetani,
Kama mbwa wa mwitu,
Atatuharibu;
Tunaitwa na Yesu
Mkombozi wetu,
Tuingie zizini,
Panapo nafasi.

Exit mobile version