Site icon Treasure Hymns- Swahili

Wimbo 104 YESU ALINIITA, NJOO nyimbo za wokovu

Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns

Wimbo 104 YESU ALINIITA, NJOO nyimbo za wokovu

 

1
Yesu aliniita, Njoo,
Raha iko kwangu,
Kichwa chako ukilaze
Kifuani mwangu
Nilikwenda kwake mara,
Sana nilichoka;
Nikapata kwake raha
Na furaha tena.

2
Yesu aliniita Njoo,
Kwangu kuna maji;
Maji ya Uzima, bure,
Unywe uwe hai.
Nilikwenda kwake mara
Na maji nikanywa;
Naishi kwake na kiu
Kamwe sina tena.

3
Yesu aliniita, Njoo,
Dunia i giza,
Ukinitangaza,
nuru Takung’arizia
Nilikwenda kwake mara,
Yeye Jua langu,
Ni kila wakati mwanga
Safarini mwangu.

Exit mobile version