Nyimbo Za Kristo – Swahili SDA Hymns
Wimbo 10 KRISTO WA NEEMA nyimbo za wokovu
1
Kristo wa neema yote
Imbisha moyo wangu,
Mifulizo ya baraka
Inaamsha shangwe kuu,
Unifunze nikupende,
Nikuandame kote,
Moyo wangu ukajae
Furaha na tumai.
2
Namshukuru sana Bwana
Aniwezesha huku,
Salama aniongoza
Hata kule nyumbani,
Yesu alinitafuta,
Njiani mbali kwake,
Akatoa damu yake
Niponywe hatarini.
3
Kweli mimi mwiwa mkubwa
Wa neema daima,
Wema wako unifunge
Zaidi kwako Bwana,
Ili nisivutwe tena,
Kukuacha e Mponya,
Nitwalie moyo wangu
uwe wako kamili.